Jumatatu, 24 Juni 2013

Nchemba, Msigwa nusura wazichape Dodoma

iv dir="ltr" style="text-align: left;" trbidi="on">
Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria, baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu

Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizozana na wabunge wa Chadema, Mchungaji Peter Msigwa(kulia)mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (wa pili kulia) na Mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (wa pili kushoto) baada ya kukutana nje ya ukumbi wa mikutano wa St Gasper,Dodoma jana wakati wa semina ya wabunge ya kuhusu Ukimwi. Picha na Fidelis Felix

Dodoma. Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha. Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria, baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu. Wabunge hao wa Chadema hawakuhudhuria kikao chochote cha Bunge kutokana na kwenda mkoani Arusha kwa shughuli mbalimbali, kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wao wa kuhitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika viwanja vya Soweto, Juni 16 jijini humo. Malumbano hayo yanatokana na Nchemba kuituhumu Chadema kuhusika na mlipuko huo, Juni 20 mwaka huu wakati akichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema chama hicho kilipanga kulipua bomu hilo ili kuwafanya Watanzania waamini kuwa Serikali ya CCM ndiyo inayohusika na tukio hilo. Ilivyotokea Wakati Msigwa akiingia katika ukumbi huo akiwa ameongozana na Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje, walikutana uso kwa uso na Nchemba ambaye alikuwa akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Said Amour Arfi. Baada ya Nchemba kumwona Msigwa alimkaribisha mchungaji huyo akisema; “Karibu sana bwana, salama lakini?” Hata hivyo, badala ya kujibu salamu hiyo ya Nchemba, Msigwa alikuja juu na kumtuhumu Nchemba kwamba anatoa kauli zinazoweza kuvuruga amani ya nchi. “Wewe ni mtu hatari sana, haya yote yanasababishwa na wewe, mnatumia damu za watu kutafuta madaraka,” alisema Msigwa akimtupia maneno Mwigulu. Baada ya kauli hiyo Nchemba alihoji akisema: “Ki-vipi? Hayo mambo tuyaache, Msigwa achana na haya mambo!” Baada ya Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM kujibu, Msigwa alimsogelea karibu na kumnyooshea kidole, huku akiendelea kumtuhumu kuwa ana siasa chafu zinazopandikiza chuki kwa jamii. Malumbano hayo pia yaliingiliwa na Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vicent Nyerere ambaye alimuunga mkono Msigwa, huku akimtuhumu Nchemba kuwa ni mtu mbaya katika siasa za Tanzania. Katika kile kilichoonekana kutaka kuweka mambo sawa, Wenje alimvuta Msigwa na kumpeleka ukumbini ili kuepusha shari baada ya wabunge hao kuzidi kurushiana maneno.

Vigogo 200 wahojiwa mabilioni ya Uswisi


Ni kuhusu mabilioni ya fedha yaliyohifadhiwa na Watanzania katika mabenki mbalimbali nchini Uswisi

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema. 

Dar es Salaam. Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara. Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa. Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge. Jaji Werema alipoulizwa na Mwananchi Jumpili maendeleo ya uchunguzi huo, alisema kuwa kazi hiyo bado inaendelea. “Uchunguzi huo unaendelea,” alisema Werema huku akisita kueleza kwa undani juu ya kazi hiyo kwa kile alichosema kuwa hana sababu ya kufanya hivyo kwa sasa. “Subiri uchunguzi bado unafanywa,” alisema Werema na alipotakiwa kueleza utamalizika lini alisema: “Utamalizika tu.” Mwanasheria huyo wa Serikali alikataa kutaja baadhi ya majina ya watu ambao tume yake imewahoji mpaka sasa. Alisema anashangazwa na swali la namna hiyo, kwa maelezo kwamba ni jambo ambalo liko wazi kuwa ni kinyume na maadili kuwataja watuhumiwa wakati huu uchunguzi ukiwa bado unaendelea. Uchunguzi huo unafanyika baada ya Benki ya Taifa ya Uswiss (SNB) kutoa taarifa mwezi Juni, 2012 kuhusu raia wa kigeni wanaomiliki akaunti za benki nchini humo. Orodha hiyo iliorodhesha pia baadhi ya Watanzania wenye akaunti zinazofikia Dola196 milioni ambazo ni sawa na Sh323.4 bilioni. Jarida la kimataifa la uchunguzi la The Indian Ocean Newsletter toleo la hivi karibuni, lilimnukuu Werema akisema uchunguzi huo kwa sasa unatia matumaini. Werema anaripotiwa akiri kuwa uchunguzi huo umefikia ‘hatua ya kutia matumaini’ na wanaendelea na kazi hiyo kwa uangalifu ili kuwa na uhakika wa taarifa wanazozitafuta. Alisema kwamba taarifa ya awali inatarajiwa kutolewa hivi karibuni na tayari idadi kubwa ya wahusika wakiwamo wabunge wameshahojiwa.

Jumamosi, 22 Juni 2013

Lipumba adai bajeti imejaa usiri


Ataka iweke wazi uchambuzi yakinifu, ni wapi fedha za miradi ya maendeleo zitatoka. Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Cuf, Profesa Ibrahimu Lipumba amesema Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2013/14, inategemea misaada kutoka nje na kwamba haionyeshi wazi upembuzi yakinifu wa miradi ya maendeleo. Pia, amesema bajeti hiyo inaonyesha kuwa deni la Taifa linakuwa kwa kasi na kufikia asilimia 50 kitu ambacho ni hatari kwa uchumi wa taifa. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akichambua baadhi ya mambo yaliyomo kwenye bajeti hiyo, Profesa Lipumba ambaye pia kitaaluma ni mchumi alisema bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14 imejaa kasoro lukuki. Alisema tatizo lililosababisha kujitokeza upungufu kwenye bajeti hiyo ni Serikali kuanza kujadili matumizi bila kujua mapato yaliyopo ni kiasi gani. “Bajeti yetu imejaa matatizo mengi, kwanza haionyeshi wazi upembuzi yakinifu kwenye miradi ya maendeleo jambo ambalo ni la ajabu,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza: “Ni jambo la kushangaza kuona bajeti ya maendeleo ambayo ndiyo muhimu kwa uchumi wa nchi inategemea mikopo ya nje, misaada ya nje na mikopo ya ndani jambo ambalo linazidi kuliongeza Taifa mzigo wa madeni.” Profesa Lipumba,alifafanua kuwa utaratibu mzuri ambao nchi nyingi za Afrika zinatumia katika kuwasilisha bajeti za nchi zao ni kujua kwanza mapato ya nchi ndipo wapange matumizi ya Serikali tofauti na sisi tunavyofanya. Profesa Lipumba alitoa mfano kuwa mara nyingi wamekuwa wakiomba kujua upembuzi yakinifu kwenye mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuja Dar es Salaam, lakini jambo hilo limekuwa gumu na limejaa usiri mkubwa. Ajira Akizungumzia suala la ajira alisema, Serikali imekuwa na kigugumizi kueleza wazi mwaka huu wa fedha imeajiri watu wangapi. Alisema “Bajeti ya mwaka jana ilieleza wazi imetoa ajira 7000, lakini mwaka huu wa Serikali imekuwa ikizunguka bila kueleza wazi itatoa ajira kiasi hagi jambo ambalo ni la kushangaza.”

Mbowe, Lema wahojiwa polisi,watoa msimamo


“Chadema tuko tayari kukabidhi ushahidi huu kwa tume huru ya uchunguzi ya Mahakama. Rais Kikwete atumie mamlaka yake ya kikatiba kuunda tume kuchunguza tukio la bomu Arusha ili ukweli ujulikane. Polisi ni watuhumiwa katika jambo hili, hivyo hawana dhamira safi na ushahidi wetu,” Arusha. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema jana, walijisalimisha Makao Makuu ya Polisi ya Mkoa wa Arusha na kuhojiwa kwa zaidi ya saa nne kabla ya kuachiwa kwa kujidhamini wenyewe huku wakitakiwa kurejea kituoni hapo, Julai 22, mwaka huu. Pia Mbowe na Lema wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuunda tume huru ya uchunguzi wa kimahakama ili kuchunguza vurugu za Arusha zilizoanza Jumamosi iliyopita baada ya bomu kurushwa kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha vifo pamoja na zile zilizofuatia wakati polisi ilipowasambaratisha wafuasi wa chama hicho kwa mabomu walipokusanyika kwenye Viwanja vya Soweto kwa lengo la kutoa heshima za mwisho kwa marehemu. Wakiongozwa na mawakili watatu, Mbowe na Lema waliwasili polisi saa 3.50 asubuhi na kuhojiwa hadi saa 9.10. Viongozi hao walipokewa na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Diwani Nyanda kabla ya kutenganishwa kwenye vyumba viwili tofauti kwa mahojiano. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mbowe, Lema na wakili Albert Msando walitaja mambo mawili ambayo polisi waliwahoji kwanza ikiwa ni ushiriki wao katika mkusanyiko usio halali kwenye Viwanja vya Soweto, Jumanne iliyopita ambao ulisambaratishwa na polisi. Jambo jingine ambalo polisi iliwahoji ni kauli yao ya kuwa na ushahidi unaohusisha polisi na tukio la bomu lililorushwa kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha vifo vya watu wanne huku zaidi ya 60 wakijeruhiwa. Mbowe alisema kwa pamoja wamewaeleza polisi kuwa hawaamini kama mkusanyiko wa Jumanne iliyopita haukuwa halali kwa sababu waliruhusiwa kuzungumza na wananchi waliokusanyika ili kuwashawishi watawanyike. “Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) wa Arusha, Gilles Mroto ndiye aliyeturuhusu kuzungumza na wananchi wale kuwataka watawanyike na ndicho tulichofanya, lakini tukashangaa kuanza kupigwa mabomu mara baada ya kuwataka watu wanaotaka kutoa heshima za mwisho kwa marehemu kwenda Hospitali ya Mount Meru,” alisema Mbowe. Alisema Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja kuwa naye aliyewaomba viongozi wa Chadema kuwatawanya wafuasi wa chama hicho baada ya kuzuiwa kutoa heshima za mwisho katika viwanja hivyo vinavyomilikiwa na Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Msimamo wa Mbowe Kuhusu ushahidi anaodai unawahusisha polisi na tukio la bomu, Mbowe alisisitiza kuwa Chadema kina ushahidi wa kutosha kuthibitisha hilo lakini alisema hakitaukabidhi mikononi mwa polisi. Alisema hakitafanya hivyo kwa kuwa jeshi hilo ni watuhumiwa wakuu hivyo hawawezi kuwa na dhamira na nia njema katika upelelezi wao. Alisema ndiyo maana badala polisi kuwaona ni msaada, kimeanza kutoa vitisho kwa wote wanaosema waliwashuhudia askari wakishambulia watu kwa risasi kabla ya kuondoka na aliyerusha bomu kwenye gari lao.

Mizengo Pinda: Nasema wapigwe tu

Lazima tuwakamate na kama katika kuwakamata watafanya jeuri, jeuri, watapigwa tu kabla ya kupelekwa tunapotakiwa kuwapeleka, kwa sababu hatuwezi kuendelea na hali hii, mkadhani kwamba tutafika tunapokwenda. Dodoma/Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameagiza vyombo vya dola kuwashughulikia kwa kuwapiga wale watakaokataa kutii amri wakati wakifanya vitendo vya uvunjifu wa amani. Akizungumza katika Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu, bungeni Dodoma jana, Pinda alisema watu wanapokaidi wanajitakia matatizo na vyombo vya dola. Alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyeuliza: “Serikali ipo tayari kiasi gani kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?” Waziri Mkuu alijibu: “Ni lilelile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria. “Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka.” Pinda alisema Serikali imedhamiria kurejesha amani nchini ikiwamo mkoani Mtwara na kuwataka Watanzania waiache Serikali ifanye kazi hiyo. Alisema Serikali ina orodha ya watu wanaosemekana kuwa ni vyanzo vya vurugu na matatizo yaliyotokea Mtwara na kushangaa wale wanaopinga kukamatwa kwao. “Lazima tuwakamate na kama katika kuwakamata watafanya jeuri, jeuri, watapigwa tu kabla ya kupelekwa tunapotakiwa kuwapeleka, kwa sababu hatuwezi kuendelea na hali hii, mkadhani kwamba tutafika tunapokwenda. Nami nasema vyombo vya dola vijipange imara vihakikishe vinadhibiti hali hii,” alisema. Hata hivyo, jibu hilo lilipata upinzani wakati Mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Said Haji alipomwuliza Waziri Mkuu: “Hapo awali umetoa kauli nzito ya kuliambia taifa hili kwamba wale raia wote, ambao watakaokuwa wakaidi wapigwe tu na watapigwa tu; naomba ninukuu Katika Ibara ya 13 na Kifungu cha 6B cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano. “Ni marufuku kwa mtu yeyote aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai kuteswa kama mtu mwenye kosa, mpaka itakapothibitika anayo hatia kwa kutenda kosa hilo. “Pia ibara hiyohiyo Kifungu cha 6 E; kinasema ni marufuku kwa mtu yoyote, kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazoweza kumdhalilisha. Kwa kauli yako uliyoitoa huoni kwamba umevunja Katiba?” Akijibu swali hilo, Pinda alisema ni lazima kutofautisha kati ya mtu aliyekwishakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria... “Mimi ninayemzungumza hapa ni mtu yule ambaye ameamua kufanya vitendo hajakamatwa na ndiyo maana nilikwambia usiandamane... hapa mahali hutakiwi kwenda wewe ukaamua kutumia mabavu kwa sababu mko wengi, ndiyo maana nikasema, hawa watu tutashughulika nao hivyohivyo.” Mbunge huyo hakuridhishwa na majibu hayo na kumtaka Waziri Mkuu kuyafuta. Hata hivyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliingilia katika na kumweleza mbunge huyo kuwa kila mtu alikuwa amemwelewa Waziri Mkuu na hakukuwa na haja ya kuendelea na hoja hiyo.

Jumatano, 19 Juni 2013

Historia ya kiburudani kuandikwa leo!


Mei 29 baada ya kifo cha marehemu Albert Mangwea, Mwana FA aliandika twitter “Sina uhakika, lakini nimeahirisha shoo yangu mpaka June 14 kama kaka tutakuwa tumeshampumzisha,” alitweet FA.Siku iliyosubiriwa kwa hamu na wadau wa muziki nchini ya tamasha la miaka 13 katika muziki ya Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee na The Finest ya mwanamuziki Khamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ imetimia leo. The Finest ya Mwana FA itafanyika pale Makumbusho jirani na chuo cha IFM, huku miaka 13 katika muziki ya Jaydee inatarajiwa kufanyika Nyumbani Lounge. Baada ya kuahirishwa Mei 31 shoo hizi mbili zote kwa pamoja zinatarajiwa kufanyika leo Juni 14 katika maeneo mawili tofauti hali inayoendelea kuwachanganya mashabiki wengi nani alitangulia kutangaza tarehe awali. Mei 29 baada ya kifo cha marehemu Albert Mangwea, Mwana FA aliandika twitter “Sina uhakika, lakini nimeahirisha shoo yangu mpaka June 14 kama kaka tutakuwa tumeshampumzisha,” alitweet FA. Lakini Jaydee aliahirisha na kusema atatangaza ni lini shoo yake itafanyika, baadaye alikuja kuandika twitter “Ni wiki ndefu kwangu Juni 13 mahakamani, Juni 14 Miaka 13 ya Jide. Juni 15 ni siku yangu ya kuzaliwa, ni Juni ni mwezi wangu,” alitweet Jide. Mwanamuziki FA amesema asilimia 15 ya mapato kutoka katika shoo hiyo, yatapelekwa kwa mama mzazi wa Ngwea. “Nimesema nitoe hela mfukoni kwangu moja kwa moja, niipeleke huku, kwa hiyo chochote nitakacho kipata, nataka kutoa asilimia 15 nimpelekee bi mkubwa,” alisema Mwana FA.

Bei ya bia, sigara zazidi kupanda


Pia bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 kwa lita hadi Sh578, sawa na ongezeko la Sh51 kwa lita. Kuhusu ushuru magari, umeongezwa kwenye magari yasiyozalisha na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka hadi asilimia 25.Dar es Salaam. Serikali imeendelea kuongeza kodi kwenye magari makuukuu, bia, vinywaji vikali, na baridi kama ambavyo kodi imekuwa ikifanya kila mwaka na kuwaathiri watumiaji. Kutokana na hali hiyo wanywaji pombe na sigara pamoja na waagizaji magari watalazimika kutumia fedha nyingi zaidi ili kupata huduma hizo. Vilevile baadhi ya bidhaa zisizokuwa za mafuta nazo zimefanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi, ikiwamo mvinyo, pombe, vinywaji vikali, na sigara. Vinywaji hivyo vimeongezwa kodi kwa asilimia 10. Kutokana na bajeti ya mwaka 2013/14 iliyosomwa jana bungeni na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, vinywaji vikali vimepanda kutoka Sh2,392 hadi Sh2,631 kwa lita, sawa na ongezeko la Sh239 kwa lita moja. Bia inayotengenezwa kwa nafaka nchini ambayo haijaoteshwa imeongezwa kodi kutoka Sh310 kwa lita hadi Sh341, sawa na ongezeko la Sh31 kwa lita. Pia bia nyingine zote zimepanda kutoka Sh525 kwa lita hadi Sh578, sawa na ongezeko la Sh51 kwa lita. Kuhusu ushuru magari, umeongezwa kwenye magari yasiyozalisha na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka hadi asilimia 25. Dk Mgimwa alisema hatua hiyo imelenga kupunguza uagizaji wa magari chakavu ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara, huku ikiongeza mapato kwa Sh510 bilioni.

Kenya yaongoza bajeti EAC

Bajeti za nchi wanachama wa nchi za Afrika Mashariki zilisomwa zote kwa muda ule ule, tukio ambalo limekuwa likifanyika kwa muda sasa.Dar es Salaam. Bajeti za nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilitangazwa jana zikitoa vipaumbele katika masuala ya usalama, afya, kilimo, elimu, nishati na kuboresha miundombinu. Bajeti hizo zilizotangazwa na mawaziri wa fedha wa nchi hizo sambamba na ile ya Tanzania, ni za Uganda, Rwanda na Kenya ambayo iliongoza kwa ukubwa wa bajeti. Bajeti hizo zilitofautiana kwa kiasi kikubwa kutokana na mahitaji na vyanzo vya mapato kwa kila nchi. Mwelekeo wa bajeti hizo pia umelenga kuongeza mapato kupitia vyanzo vya ndani kwa kuongeza ushuru na kodi kwenye vileo, vyombo vya usafiri na bidhaa za anasa. Kenya Sh28.5 trilioni Waziri wa Fedha wa Kenya, Henry Rotich alisema kwamba Bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2013/14 itafikia Sh1.5 trilioni za Kenya (sawa na Sh28.5 trilioni za Tanzania). Bajeti hiyo ilisomwa jana bungeni jijini Nairobi, ndiyo ya kwanza kwa Rais Uhuru Kenyatta aliyechukua madaraka hivi karibuni. Moja ya ameneo muhimu yaliyopewa kipaumbele katika bajeti hiyo ni elimu, ambapo Sh17.4 bilioni (Sh330.6 bilioni za Tanzania) zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha mkakati wa Serikali ya Jubilee wa kununua kompyuta ndogo 1,300,000 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi. Uganda Sh7.2 trilioni Waziri wa Fedha wa Uganda, Maria Kiwanuka ametangaza Bajeti ya Serikali ya nchi hiyo kwa mwaka wa Fedha 2013/14 ambapo ambapo Sh 12 trilioni (sawa na Sh7.2 trilioni za Tanzania) zitatumika. Bajeti hiyo inategemea vyanzo vya ndani vya mapato baada ya misaada ya wafadhili kushuka kwa zaidi ya asilimia 93, kutoka Sh749 bilioni (za Uganda) mwaka 2012/13 hadi Sh50 bilioni za Uganda mwaka 2013/14. Kiwanuka alisema katika mwaka huu wa fedha, wafadhili wamesaidia asilimia 25 ya bajeti ya nchi hiyo lakini katika mfumo wa mikopo na kufadhili miradi, ambapo matumizi ya Serikali yatafikia Sh8.4 trilioni za Uganda.

CHEGGE ‘aichanachana’ BAJETI YA SERIKALI 2013/14

Kamati ya Bunge ya Bajeti inasema wizara zinatumia zaidi fedha ambazo zimeidhinishwa na Bunge.Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge, amesema mwelekeo wa matumizi ya Serikali hauridhishi na kuainishisha changamoto mbalimbali, ikiwamo ongezeko la safari za viongozi na watendaji wa Serikali. Chenge alisema safari za nje zimeongezeka kwa asilimia 12, wakati zile za ndani zina ongezeko la asilimia 18. Alibainisha hayo alipowasilisha taarifa ya kamati yake kuhusu hali ya uchumi kwa mwaka 2012 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2013/14, tathmini ya utekelezaji Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13 na mapendekezo ya mapato na matumizi ya Serikali. “Mwelekeo wa matumizi ya Serikali hauridhishi. Lipo tatizo katika matumizi ya mafuta na vilainishi serikalini. Tathmini inaonyesha Serikali inatarajia kutumia fedha nyingi zaidi,” alisema Chenge na kuongeza: “Kununua mafuta katika mwaka ujao, ikilinganishwa na mwaka huu wa fedha. Ongezeko hilo linafikia asilimia 19.” Kwa mujibu wa Chenge, bajeti ya Serikali mwaka hadi mwaka zimekuwa zikitumika kwa kiasi kikubwa kulipa madeni, badala ya kutekeleza mipango iliyopangwa mwaka husika. Alisema matokeo yake, miradi haikamiliki kwa wakati na kuiongezea gharama Serikali, alitaka kufanya jitihada za makusudi kudhibiti hali hiyo. Alifafanua kuwa kuna tatizo kubwa la malimbikizo la madeni kwa wizara na idara za Serikali, huku asilimia 70 ya bajeti inayopitishwa ikitumika kulipia madeni. Chenge alisema kamati yake imebaini kuwapo kwa baadhi ya wizara, zinazotumia fedha nyingi zaidi ya zinazoidhinishwa na Bunge. Alisema Julai 2012 hadi Aprili 2013, Serikali ilikopa Sh1.364.7 bilioni kutoka soko la ndani la mitaji.

Jumanne, 18 Juni 2013

Upinzani washindwa kuwasilisha bajeti

Sasa kwa kuwa hawapo nitawataja wabunge kadhaa kwa ajili ya kuchangia hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2013/14.Dodoma. Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, imeshindwa kuwasilisha hotuba mbadala ya bajeti kama ilivyo kawaida, baada ya wabunge wote wa Chadema kutohudhuria. Wabunge hao walielezwa kuwa wapo mkoani Arusha kufuatilia mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita, eneo la Soweto na kuua watatu wawili na kujeruhi 70. Tukio hilo ambalo ni la kwanza kutokea, lilitokea baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge kuwasilisha taarifa yake kuhusu hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka 2013 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2013/14 na tathmini ya utekelezaji Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13. Baada ya Chenge kumaliza uwasilishaji wake, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliita msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Fedha (Zitto Kabwe), hata hivyo hakuwapo. “Baada ya Chenge kumaliza ilikuwa zamu ya upinzani kuwasilisha bajeti yao, lakini siwaoni na sina taarifa rasmi za kutokuwapo kwao leo wala sijapokea simu,” alisema Makinda alisema na kuongeza: “Sasa kwa kuwa hawapo nitawataja wabunge kadhaa kwa ajili ya kuchangia hotuba ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2013/14.” Hata hivyo, baadaye Kambi Rasmi ya Upinzani ilisambaza kwa waandishi wa habari hotuba yake mbadala ya bajeti iliyokuwa isomwe bungeni na Zitto, ambayo Msemaji wa Chadema, John Mnyika alithibitisha kuwa sahihi. Katika hotuba hiyo, Zitto licha ya mambo mengine, Serikali ya CCM imechukua na kuyafanyia kazi na kuleta matokeo mazuri. Alisema kwamba Kambi Rasmi ya Upinzani itaendelea kuionyesha njia Serikali na CCM kuhusu namna bora na rahisi ya kuondoa nchi katika giza la uchumi na lindi la umaskini. Zitto alisema deni la taifa limeendela kuwa changamoto. kubwa kwa uchumi, hali inayosababisha bajeti ya Serikali kuendelea kuwa tegemezi, hivyo kushindwa kutatua kero za uchumi wa wananchi.

Mtoto: Nilipigwa risasi na polisi

Wakati majeruhi wametuhumu polisi kutumia risasi za moto, nayo Serikali imetangaza donge la Sh100 milioni kwa atakayemfichua mlipuaji wa bomu Arusha. Arusha/Dodoma. Wakati watu waliofariki kwenye tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa Chadema ikifikia watatu baada ya jana kufariki kwa mtoto Amir Ally (7), mtoto mwingine wa miaka kumi na moja aliyejeruhiwa, amedai kwamba alipigwa risasi na polisi kwenye tukio hilo. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye ametoa tamko kuwa chama chake kina ushahidi wa kutosha wa watu waliohusika na tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa kampeni wa chama hicho. Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Arusha Medical Lutheran Center (ALMC), Dk Paul Kisanga alisema jana kuwa, Amir alifariki jana asubuhi baada ya kupata majeraha makubwa kichwani yaliyodhuru ubongo wake. Dk Kisanga alisema huyo ni mmoja wa watoto watano, waliojeruhiwa wakati wakitoka madrasa huko Kaloleni, jirani na Uwanja wa Soweto kulipokuwa na mkutano na alifariki jana asubuhi hospitalini hapo. Alisema watoto wengine wawili ambao ni ndugu; Fatuma na Sharifa Jumanne wamepelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi baada ya miili yao kukutwa na vyuma. Dk Kisanga aliwataja watoto wengine waliojeruhiwa kuwa ni Fahad Jamal (7) ambaye yupo ICU akisubiri timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na hali yake kutoruhusu kusafirishwa. Pia yupo Abubakar Adam (11) ambaye amejeruhiwa mguuni na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa, Mount Meru. Mtoto aeleza kupigwa risasi Adam alisema jana kuwa alipigwa risasi na mtu aliyekuwa amevalia sare za polisi, wakati akitoka madrasa akiwa na ndugu yake, Fahdi katika eneo la Soweto. Alisema akiwa njiani, aliona watu wakimkimbiza mtu na ghafla alishangaa kupigwa risasi na kuanguka chini. “Namkumbuka aliyenipiga risasi alikuwa amevaa sare za polisi,” alisema Adam mwanafunzi katika Shule ya Msingi Levolosi huku akitokwa machozi. Muuguzi wa zamu, katika katika wodi ya watoto katika Hospitali ya Mount Meru, Asha Semdeli alisema jana kuwa mtoto huyo ana vyuma viwili katika mguu wake. “Tunasubiri afanyiwe upasuaji kwani tayari mashine ya X-ray inaonyesha vyuma kuwepo katika mguu wa Adam siwezi kusema ni risasi au la,” alisema Semdeli.

Jumatatu, 17 Juni 2013

CCM yazoa viti vingi vya udiwani

Nassari alivamiwa, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini na watu wanaodaiwa kuwa viongozi na wafuasi wa CCM. Chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika sehemu mbalimbali ziligubikwa na vurugu wakati hali ilikuwa mbaya zaidi huko Makuyuni mkoani Arusha ambako Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alipigwa na wafuasia wa CCM na kulazimika kulazwa hospitalini. Pamoja na vurugu hizo, CCM iliendelea kudhihirisha umwamba wake katika ulingo wa siasa baada ya kujizolea viti vingi vya udiwani wakati wa chaguzi ndogo zilizofanyika sehemu mbalimbali nchini. Wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa walikuwa wanafuatilia kwa kina chaguzi hizo ili kupima joto la kisiasa nchini. Uchaguzi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni ule wa Makuyuni wilayani Monduli ambako Mbunge wake ni mwanasiasa maarufu Edward Lowassa. CCM iliibuka kidedea huko Makuyuni na kufanya maneno ya Rais Jakaya Kikwete kuwa Lowassa ana misuli ya kuifanya CCM ishinde huko Monduli. Lowassa alikuwa na kibarua cha kukabiliana na Chadema waliokuwa wanataka kujipenyeza Monduli ambako hawajahi kuwa na kata tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe. Hata hivyo, bado CCM haijapata dawa ya ushindi Pemba kwani kilishindwa vibaya na CUF kwenye uchaguzi wa ubunge wa Chambani. Chadema kwa upande wake kilitoa changamoto kwa CCM katika chaguzi hizo za kata na hata kujizolea kata mbili za Iyela huko Mbeya na wilayani Hanan’g huko mkoani Manyara. Nassari apata kichapo Makuyuni Nassari alivamiwa, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini na watu wanaodaiwa kuwa viongozi na wafuasi wa CCM, akiwa katika harakati za uratibu wa shughuli za upigaji kura za udiwani katika Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli. Nassari aliyekuwa wakala mkuu wa Chadema katika kata hiyo alivamiwa na kundi la watu zaidi ya 30 waliomshambulia kwa fimbo na Tukio hilo lilitokea jana kati ya Saa 3:00 na 4:00 katika kituo cha kupigia kura cha Kwa Zaburi wakati mbunge huyo alipofika kuangalia maendeleo ya zoezi la kura.

Jumapili, 16 Juni 2013

POLISI YATUMA TIMU KUCHUNGUZA BOMU MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA

KUFUATIA mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kuuwa watu wawili na majeruhi zaidi ya 60 katika mkutano huo, Jeshi la Polisi Nchini limeunda timu ya maofisa kutoka makao makuu Dar es Salaam ili kuongeza nguvu ya uchunguzi wa mlipuko wa bomu hilo. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP. Said Mwema amesema imeteua maofisa hao ili kwenda kuongeza nguvu za uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo la mlipuko wa bomu uliotokea Soweto, Kata ya Kaloleni Arusha. Alisema timu hiyo ya uchunguzi inayoenda kusaidiana na wengine kutoka Mkoani Arusha, inajumuisha makamishna wawili kutoka Operesheni na Idara ya Upelelezi Makao Makuu, itaongozwa na Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo, Paul Chagonja na Kamishna Issaya Mngulu kutoka Idara ya Upelelezi Makosa ya Jinai. Jeshi la Polisi mbali na kulaani kitendo hicho ambacho kinaashiria vitendo vya kigaidi, linaendesha oparesheni nchini nzima ya kubaini wafadhili na wahusika wanaopanga matukio hayo ya kinyama. Aidha IGP amewaomba wananchi wote wenye taarifa zozote juu ya tukio wawasiliane moja kwa moja na IGP Mwema kwa namba 0754 78 55 57 au katika kituo chochote cha Polisi. Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza leo amesema uchunguzi wa tukio hilo unahusisha vikosi vyote vya usalama nchi likiwemo Jeshi la Wananchi (JWTZ) kubaini wahalifu hao ambao wanatishia usalama wa nchi na raia wake. Hii ni mara ya pili kwa mlipuko wa bomu la kurushwa unatokea Mkoani Arusha katika mkusanyiko wa watu kwani hivi karibuni ulitokea mlipuko mwingine wa bomu katika moja za Parokia za Kanisa Katoliki mkoni humo.

UGAIDI TENA ARUSHA, BOMU LAJERUHI NA KUUA

Bomu hilo lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi.Arusha. Mkutano wa Chadema wa kumaliza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani mjini Arusha, jana ulivunjika baada ya bomu kulipuka na kuua watu wanne na wengine kujeruhiwa. Bomu hilo lililipuka jana saa 11:50 dakika chache kabla ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano huo uliofanyika katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi. Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka katika mkusanyiko wa watu, Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini Arusha na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa. Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru Frida Mokiti alisema katika hospitali yake kuna maiti moja ya mtoto na majeruhi 11. Habari zingine zilisema katika hospitali ya Misheni ya Selian kuna maiti za watu wawili, waliokufa kutokana na shambulio hilo na majeruhi ambao idadi yao haijafahamika. Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema katika tukio hilo watu wawili wamepoteza maisha, mwanamke na mwanamume na kwamba idadi ya majeruhi bado haijafahamika kwa kuwa wametawanywa katika hospitali mbalimbali mkoani humo. Watu walioshuhudia tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa bomu hilo lililipuka karibu na jukwaa walilokuwa wamekaa viongozi wa Chadema, wakati Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wakiwa katika hatua za kumaliza kuhutubia. Taarifa zilidai kuwa kuna mtu alionekana akirusha kitu kinachodaiwa bomu kwenye eneo la jukwaa karibu na gari la matangazo la chama hicho, lakini alipokuwa akifuatiliwa baada ya kutokea mlipuko huo, polisi nao walikuwa wameanza kudhibiti watu kwa kulipua mabomu ya kutoa machozi na kupiga risasi za moto hali iliyozidisha taharuki. Baada ya tukio hilo watu waliokuwa katika mkutano huo walitawanyika wakikimbia kuokoa maisha yao huku wakimwacha Mbowe na Lema na viongozi wengine wakiwa bado wako jukwaani. Hali hiyo ilifanya barabara zote za mji wa Arusha kujaa watu waliokuwa wakikimbia ovyo. Hali hiyo ya watu kukimbia ovyo kuliwafanya askari polisi wengi kuingia mitaani kudhibiti watu na hivyo nao kulazimika kutumia mabomu ya machozi hali ambayo ilizidisha taharuki. Baadhi ya watu waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na wengine katika Hospitali ya Seliani na wafuasi wa Chadema na watu wengine waliokuwa katika eneo hilo.

Jumamosi, 16 Machi 2013

US TOBOOST NUCLEAR MISSILE DEFENCE TO COUNTER N KOREA

Chuck Hagel: "The American people should be assured our interceptors are effective" The US plans to bolster its missile defences on the west coast to counter the threat from North Korea, Defence Secretary Chuck Hagel has announced. He said the US would add 14 interceptors, which can shoot down missiles in flight, to 30 already in place in California and Alaska by 2017. Mr Hagel cited a "series of irresponsible and reckless provocations" recently by North Korea. Pyongyang carried out a third nuclear test last month. A statement in North Korean state media last month also threatened the US with a pre-emptive nuclear strike. Europe plan shelved However, analysts say the regime is years away from producing a missile capable of carrying a nuclear warhead to the US. "The US has missile defences to protect us from limited ICBM [Inter-Continental Ballistic Missile] attacks," Mr Hagel told Friday's press conference. "But North Korea in particular has recently made advances in its capabilities and has engaged in a series of irresponsible and reckless provocations." The defence secretary said the US needed to "stay ahead of the threat". North Korea has recently ramped up anti-US rhetoric He said the additional 14 interceptors would be deployed to Fort Greely in Alaska at a cost of about $1bn (£660m). As part of the strategy, the US will also deploy a radar-tracking station in Japan. The Pentagon will shift some of the funding away from the missile defence programme it has been setting up in Europe. Mr Hagel said US commitment remained "ironclad" to the European shield, and that missile batteries would be established in Poland and Romania by 2018. But he said the another part of the plan had been shelved. James Miller, Principal Deputy Under Secretary for Policy at the Department of Defence, later clarified that the final phase of the missile defence programme had been dropped. "The prior plan had four phases. The third phase involved the deployment of interceptors in Poland. And we will continue with phases one through three," Mr Miller told reporters. "In the fourth phase, in the previous plan, we would have added some additional type of interceptors - the so-called SM-3 IIB would have been added to the mix in Poland. "We no longer intend to add them to the mix, but we'll continue to have the same number of deployed interceptors in Poland that will provide coverage for all of Nato in Europe," he added. President George W Bush first proposed a defence shield in Europe, which had incensed Russia. His successor Barack Obama rolled back on the plans, announcing a much smaller deployment. Friday's announcement represents a further toning down of the plans. The Pentagon said its top North Korea official would be visiting Russia and Germany next week. The Alaska and California sites were built during the presidency of George W Bush as protection from a possible strike by North Korea. Technical difficulties with the interceptors slowed their installation. When asked about the "poor performance" of interceptors during recent trials, Mr Hagel said further tests would be carried out this year. "We have confidence in our system," he said, "and we certainly will not go forward with the addition of the 14 interceptors until we're sure we have the complete confidence we need."

Jumatano, 20 Februari 2013

Jumapili, 17 Februari 2013

Museveni's shame over African 'failure' in Mali

Uganda's President Yoweri Museveni has been speaking to BBC Africa about the military intervention in Mali. He feels that the role of African armies has been more than disappointing. "To find that the Africans cannot defend their own territory, is a big shame," he told the BBC's Alan Kasujja

Same-sex parent: 'We wanted our own children

When the Welsh Secretary David Jones suggested that same sex couples could not provide a 'warm and safe environment' for bringing up children it caused widespread anger. He has since tried to clarify his comments by saying he is not opposed to gay partners raising children but thinks marriage should be reserved for heterosexual couples. Natalie Drew, who has two children with her partner, Ashling Philips, said it was all about equality and providing a good, loving home for them.read more... Hakuna maoni:

no homo

no homo: no homo

Meek Mill - House Party ft. Young Chris

Jumapili, 10 Februari 2013

THE LURE OF NEW YORK'S RAILWAYS

The lure of New York's railways As Grand Central Station celebrates its 100th birthday, David Cannadine looks back at its history, including how Jacqueline Kennedy Onassis helped save it from destruction

Premier League football Live text commentary as Manchester United host Everton in the Premier League after Aston Villa hold on to beat West Ham

Premier League football Live text commentary as Manchester United host Everton in the Premier League after Aston Villa hold on to beat West Ham

Holiest day at India's Kumbh Mela The most auspicious day of bathing is held at India's Kumbh Mela pilgrimage, and officials say some 30 million people have already taken a dip

Holiest day at India's Kumbh Mela The most auspicious day of bathing is held at India's Kumbh Mela pilgrimage, and officials say some 30 million people have already taken a dip

Stripped bare With one in three young Italians currently jobless, the fear of unemployment haunts a generation. The BBC's Alan Johnston meets the men for whom The Full Monty has become a political statement

Stripped bare With one in three young Italians currently jobless, the fear of unemployment haunts a generation. The BBC's Alan Johnston meets the men for whom The Full Monty has become a political statement

Challenging chalga Bulgaria's sex-soaked pop-folk music culture has come under scrutiny following a controversial decision to award EU money to a top producer

Challenging chalga Bulgaria's sex-soaked pop-folk music culture has come under scrutiny following a controversial decision to award EU money to a top producer

Amazing Rolls royce in THE WORLD

FANTASTIC ROLLS-ROYCE CONCEPT CAR

Vampire diaries....... Download your free episode here

download the best latest game

http://kat.ph/cities-xl-platinum-multi7-steam-rip-cracked-rg-gameworks-t7074251.html/>